Maafisa wa polisi wanamsaka mwanaume ambaye anashukiwa kumuua nduguye kufuatia ugomvi juu ya mahindi katika kaunti ya Kakamega.

Inadaiwa mshukiwa Robinson Munyenya mwenye umri wa miaka 32 alimuaa nduguye mwenye umri wa miaka 41 kufuatia ugomvi baina yao, akimshtumu marehemu kwa kuiba mahindi kutoka kwa nyuma yake.

Juhudi za baba yao kuwatengansiha ziliambulia patupu, huku marahemu akifarki wakati alikimbizwa hospitalini kupokea matibabu.