Wanafunzi wote watarejea shuleni tarehe nne Janauri mwaka ujao kwa muhula wao wa pili.

Tangazo hili limetolewa na Waziri wa Elimu Profesa George Magoha, kuashiria kuwa hakuna mwanafunzi ambaye atarudia darasa huku muhula huo wa pili ukitarajiwa kukamilika tarehe 19 Machi mwaka huu.

Magoha atoa hakikisho kwa taifa kuwa wanafunzi watakuwa salama wakiwa shuleni kwani mikakati yote ya kuzuia maambukizi ya corona shuleni imewekwa ikiwemo kuwanunulia wanafunzi barakoa.