Bingwa wa mbio za olimpiki Conseslus Kipruto ameachiliwa kwa dhamana ya Sh200, 000 na mahakama ya Kapsabet baada ya kukanusha mashtaka ya ubakaji.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka Ishirini na tano anatuhumiwa kumbaka msichana wa umri wa miaka kumi na tano kati ya Octoba 20 na Ocoba 21 katika kijiji cha Tironin kaunti ya Nandi.

Wazazi wa msichana huyo walipiga ripoti kwa Polisi baada ya mwanao kutoweka kwa muda wa siku tatu na kwenda kuishi na mwanariadha huyo nyumbani kwake Chesumei.

Kipruto alishinda nishani ya dhahabu kwa wanaume katika mbio za 3,000m kuruka viunzi na maji katika mashindano ya olimpiki yaliyoandaliwa nchini Uchina, 2016.

Bingwa huyo hakukomea hapo kwani alishinda mbio za dunia mwaka 2017 na 2019 zilizoandaliwa mjini London na Doha mtawalio.