Naibu Rais William Ruto ameonekana kuuunga mkono viongozi kutoka jamii ya wafugaji, baraza la kidini nchini NCCK, baadhi ya makundi ya wanawake na baadhi ya maseneta ambao wanataka ripoti ya BBI kufanyiwa marekebisho.

Katika taarifa kupitia kwa mtandao wa Twitter, Ruto anasema ni kinaya kutaka katiba kufanyiwa marekebisho lakini kupinga ripoti ya BBI kurekebishwa.

Dr Ruto amelalamikia kile anasema ni kujenga kuta za kuwazuia wengine katika harakati za kujenga madaraja ya kuwaunganisha wakenya wote.

Naibu Rais amekuwa kwenye mstari wa mbele kuapa kuipinga ripoti ya BBI iwapo haitajumuisha kile anasema ni masuala yanayomuathiri mwananchi wa kawaida.