Aliyekuwa muwaniaji wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Kakamega Mabel Muruli amefariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wa corona.

Gavana wa kaunti hiyo Wycliffe Oparanya ambaye amedhibitisha kifo hicho amemtaja marehemu kama mtu mwenye bidii katika utendakazi wake.

Kifo cha Muruli kinakuja siku moja baada ya mkuu wa wafanyikazi katika kaunti hiyo Robert Sumbi kufariki kutokana na ugonjwa wa COVID19.

Sumbi alipoteza maisha akipokea matibabu katika hospitali kuu ya Kakamega wiki moja baada ya kupatikana na ugonjwa huo.

Marehemu ni kati ya wafanyikazi waliokutwa na virusi hivyo hali ambayo imesababisha gavana Oparanya kufunga makao makuu ya afisi za kaunti hiyo.