Wakenya watatumia kima Sh14b kuandaa kura ya maamuzi imesema tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.

Kaimu afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Hussein Marjian anasema tume hiyo imefanya makadirio hayo kwa kuzingatia uwezekano wa kufanyia katiba marekebisho kupitia mchakato wa BBI.

Ameongeza kuwa wamezingatia kiasi hicho kutokana idadi ya wapiga kura ambayo ni 19.6M ila amesema idadi hiyo itaongezeka kutokana na shughuli inayoendelea ya kuwasajili wapiga kura.

IEBC vile vile imesema tayari inajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa 2022 na kura ya maamuzi.