Tume  ya kuwaajiri walimu nchini TSC  imewapongeza walimu  kwa kuwa  kwenye mstari  wa mbele kuwapa wanafunzi mafunzo mbalimbali ya kujikimu kimaisha na pia kutoa hamasisho kuhusiana na janga la korona.

Licha ya kuripotiwa kuongezeka kwa visa vya mimba za mapema baada ya shule kufungwa, afisa mkuu mtendaji wa TSC Dr Nancy Macharia amempongeza mwalimu Elizabeth Kadzo aliyemwokoa mtoto wa kike kutoka kwa ndoa ya mapemakaunti ya  Mombasa.

Walimu wengine waliopongezwa ni Joel Kariuki kwa kuwaelimisha wanafunzi juu ya masomo ya sanaa kaunti ya nyeri, Stephene Onditi ambaye aliwaelimisha wanafunzi ufugaji wa  kuku kaunti ya Homabay na Ben Owiti aliyewaleta pamoja wanafunzi kushiriki mchezo wa kandanda katika kaunti ya kisumu miongoni mwa walimu wengine.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa (TSC )Dr Lydia Nzomo amewapongeza walimu kwa kutokana na mchango wao kwenye jamii haswa wakati huu ulimwnegu unapambana na janga la corona.

Naye Katibu mkuu wa chama cha walimu nchini KNUT Wilson Sossion ameishtumu TSC kwa madai ya kuwanyanyasa walimu kwa kutojali mashalhi yao ikiwemo kuwapandisha vyeo walimu wenye masomo ya juu.

Tumezungumza na baadhi ya walimu ambao wameelezea kujivunia kwao katika taalum yao.

Maadhimisho ya mwaka huu ni tofauti kwani yanawadia wakati ambapo kalenda ya masomo imesambaratishwa na janga la corona.

Humu nchini Kenya, hii ni wiki ya pili sasa walimu wako shuleni bila wanafunzi baada ya shule kufungwa Mwezi Machi kuzuia maambukizi ya corona.