Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi atafahamu hii leo iwapo ataachiliwa kwa dhamana baada yake kukanusha mashtaka ya uchochezi.

Hakimu mkuu wa Mahakama ya Nakuru Josephat Kalo anatazamiw akutoa uamuzi wa ombi la upande wa mashtaka kutaka kumzuilia Sudi kwa siku kumi na nne zaidi kukamilisha uchunguzi dhidi yake.

Hata hivyo Sudi anataka kuachiliwa kwa dhamana na kuahidi kuwa hatahitilafiana na ushahidi na kuwa hawezi kutoroka ikizingatiwa kuwa hadhi yake ya ubunge.

Mbunge huyo pia anakabiliwa na mashtaka ya kukataa kukamatwa, kumdhulumu afisa wa polisi na kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Sudi anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Nakuru baada yake kukanusha mashtaka ya uchochezi.