Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi atazuiliwa katika kituo cha kati cha Nakuru kwa siku saba zaidi kuruhusu kukamilika kwa uchunguzi kuhusu madai ya kutumia matamshi ya chuki.

Upnade wa mashtaka ulikuwa umeiomba mahakama kuruhusu mbunge huyo kuzuiliwa kwa siku kumi na nne zaidi kutoa nafasi kwa uchunguzi baada yake kukanusha mashtaka ya uchochezi.

Sudi alikuwa ameiomba mahakama kumuachilia kwa dhamana ambapo alikuwa ameahidi kuwa hatahitilafiana na ushahidi na kuwa hawezi kutoroka ikizingatiwa kuwa hadhi yake ya ubunge.

Mbunge huyo pia anakabiliwa na mashtaka ya kukataa kukamatwa, kumdhulumu afisa wa polisi na kumiliki silaha kinyume cha sheria.