Maseneta wamemshambulia vikali kwa maneno mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya kwa kufunga kaunti kutokana na mgogoro wa kifedha.

Maseneta wakiongozwa na Johnson Sakaja wa Nairobi na mwenzake wa Makueni Mutula Kilonzo Jr. wamemsuta Oparanya kwa kushindwa kuonesha uongozi wakati ambapo taifa linashuhudia mgogoro.

Na licha ya kushindwa kuelewana kuhusu mfumo utakaotumika katika kugawa pesa katika serikali za kaunti, maseneta wametishia kumuita gavana Oparanya kufika mbele yao iwapo Wakenya watakosa huduma muhimu kuanzia kesho kufuatia hatua hiyo ya baraza la magavana.

Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutua amesema atakuwa wa kwanza kufunga shughuli za kaunti kuanzia Alhamisi hii.