Naibu rais William Ruto amewasihi wanasiasa kukomesha siasa zilizojikita katika misingi ya ukabila na zinazolenga kuwagawanya Wakenya.

Badala yake naibu amewataka viongozi kuendeleza siasa kwa kuzingatia sera na wala sio chuki.

Ruto amesema haya baada ya kuwakaribisha viongozi wa kidini kutoka Narok sawa na wanasiasa wakiwemo wabunge Lemanken Aramat (Narok Mashariki), Gabriel Tongoyo (Narok Magharibi) na mwakilishi wa wanawake Narok Soipan Tuya.