Mbunge wa Kandara Alice Wahome ameishtaki serikali kufuatia hatua ya kumruhusu mkurugenzi wa shirika linalosimamia huduma za Nairobi (NMS) Meja Jenerali Mohammed Badi kuhudhuria vikao vya mawaziri.

Kwenye kesi yake, Wahome anataka Badi kuzuiliwa kuhudhuria mikutano ya baraza la mawaziri kwa misingi kuwa hatua hiyo ya rais Uhuru Kenyatta inakiuka katiba.

Badi yuko huru kuhudhuria mikutano ya mawaziri baada ya kula kiapo cha siri katika Ikulu ya rais juma lililopita.

Taarifa kutoka ikulu iliarifu kuwa hatua hiyo inazingatia sheria iliyoruhusu serikali kuu kutwaa baadhi ya majukumu ya serikali ya kaunti ya Nairobi.