Maafisa wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini (EACC) wamefanya upekuzi katika makao makuu ya taasisi ya kusambaza dawa na vifaa vya matibabu (KEMSA), Nairobi wakati ambapo uchunguzi kuhusu tuhuma za ufisadi katika shirika hilo unaendelea.

Upekuzi katika makao hayo ya KEMSA umefanyiko kwa makusudi ya kutafuta stakabadhi muhimu zitakazosaidia katika uchunguzi unaoendelea kuhusu ununuzi wa vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Milango ya KEMSA imefungwa wakati wa upekuzi huo asubuhi huku wafanyikazi wakiamrishwa kusalia ndani ya afisi zao.

Haya yanajiri siku moja baada ya maafisa wa taasisi hiyo kuhojiwa katika makao makuu ya EACC, Nairobi kuhusiana na sakata hiyo.