Tanzania imetangaza kupiga marufuku ndege za Kenya kuingia kwenye anga zake baada kufungiwa nje kwenye orodha ambayo raia wake wanaruhusiwa kuingia Kenya kufuatia kurejelewa kwa safari za ndege za kimataifa.

Mamlaka ya angani Tanzania (TCAA) katika taarifa imesema inajibu hatua ya Nairobi kuruhusu ndege kutoka Dar/Kilimanjaro/Zanzibar kuanzia Agosti 1.

Haya yanajiri saa chache baada ya Kenya kuongeza mataifa saba kwenye orodha ya nchi ambazo raia wake wataruhusiwa kuingia katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Mataifa hayo ni pamoja na Marekani (bila kuwepo kwa raia kutoka majimbo ya California, Florida & Texas); Ugengereza, Ufaransa, Uholanzi, Qatar, Milki za Kiarabu na Italia.

Mbali na hayo, mataifa mengine ambayo raia wake wataingia Kenya ni China, Zimbabwe, Korea Kusini, Japan, Canada, Ethiopia, Switzerland, Rwanda, Uganda, Namibia na Morocco.