Mary Wanyonyi Mkewe aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC Wafula Chebukati ameapishwa mapema hii leo kama mwenyekiti mpya wa tume ya Ugavi wa Rasilimali CRA.
Wanyonyi ameapishwa hii leo na Jaji Mkuu katika hafla iliyoandaliwa katika majengo ya mahakama ya Rufaa.
Kuapishwa kwa wanyonyi kunakuja baada ya kuidhinishwa na bunge la Kitaifa kugfuatia uteuzi wake na Rais William Ruto.
Wanyonyi atamridhi Jane Kirngai aliyestaafu baada ya kuhitimisha muhula wake wa miaka sita.
Akihojiwa na Kamati ya Bunge la Taifa kuhusu Fedha na Mipango ya Taifa Mary chebukati aliiambia wabunge kuwa uteuzi wake haukuchochewa kwa njia yoyote na kuwa yeye ni mke wa aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC.
“Ninajivunia kwamba Wafula Chebukati ni mume wangu. Ninajivunia kuwa yeye ni baba wa watoto wangu. Ninajivunia kuitwa Mary Wanyonyi, Mary Wafula au hata Mary Chebukati ’’ Alisema Mary.
Alichaguliwa miongoni mwa watu watatu waliopendekezwa akiwemo Thomas Ludindi Mwadeghu na Felicity Nkirote Biriri.
Wanyonyi ni Mhasibu Aliyeidhinishwa na Mpatanishi Aliyeidhinishwa na Ana Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara na Shahada ya Biashara (Uhasibu).
.