CHERARGEI

Seneta wa Nandi Samson Cherargei ameikosoa Mahakama Kuu kuhusu uamuzi wa kuharamisha uteuzi wa Makatibu Waandamizi 50.

Benchi la majaji watatu katika uamuzi wake ulisema kuwa sheria haikufuatwa katika mchakato wa kubuni nafasi hizo.

Katika taarifa, Cherargei alisema Mahakama Kuu iliharamisha teuzi hizo kinyume na katiba bila kuzingatia uhalali wa kesi hiyo.

https://twitter.com/scherargei/status/1675854497430528000

Cherargei amefichuwa kuwa serikali inania ya kukataa rufaa uamuzi huo ambao umeonekana kama pigo kubwa kwa Rais William Ruto.

“Tutakata rufaa dhidi ya uamuzi huu ambao unakanusha maslahi ya umma na kanuni za Haki Asili. Nani atamtazama mlinzi?” Alisema Cherargei.

Majaji Kanyi Kimondo, Hedwig Ong’udi na Ali Visram walikubaliana na walalamishi katika kesi hio kwamba hakukuwa na ushirikisho wa umma kuhusu nafasi 27 za ziada.

Majaji hao walisema kuwa tume ya Huduma ya PSC ilisaka maoni ya umaa kubuni nafasi 23 tu ila Rais Ruto akateuwa CAS 50.

“Utaratibu uliofuatwa kubuni nafasi 27 za ziada haukuzingatia ushiriki wa umma. Mchakato huo haukuafiki matakwa ya Katiba,” benchi iliamua.

Kesi ya kupinga uteuzi wa CAS uliwasilishwa na chama cha mawakili Humu Nchini LSK, Shirika la Katiba Institute na Mkenya anayeishi Ughaibuni Eliud Matinda