Ni pigo kwa makatibu waandamizi 50 walioteuliwa na Rais William Ruto miezi michache iliyopita baada ya mahakama ya upeo kutoa uamuzi wake kuwa uteuzi wao unakiuka katiba na kuwa ni ubadhirifu wa mali ya umma

Akitoa uamuzi huo jaji Hedwig Ongundi amesema uteuzi wao haukufuata taratibu zinazofaa Kwa mujibu wa katiba

Kulingana na mahakama, hatudhani kwamba ni halali kikatiba kuwateua  makatibu 50 kuwa wasaidizi wa mawaziri ishirini na wawili pekee,Jaji Hewdig alisema

Kimondo akisisitiza kuwa maoni yaliyokusaywa kutoka kwa wakenya yalilenga uteuzi wa makatibu waandamizi 23 pekee

”Katika taarifa iliyotolewa tarehe 11/09/2022 , Daktari Joseph Kinyua alikuwa  ameamrishwa na RAIS kutangaza  nafasi 23 pekee za wazi kwa makatibu waanadamizi”

Kesi dhidi ya uteuzi wa makatibu hao iliwasilishwa mahakamani  na Mkenya kwa jina Eluid Matinde, chama cha wanasheria nchini (LSK) na shirika la Katiba Institute

Aidha jaji mkuu Martha Koome aliteua Jopo la Majaji  watatu, Alim Visram Kanyi Kimondo na Hedwig Ongundi ili  kusikiliza kesi ya kupinga uteuzi wa makatibu hao,ambao  mahakama ilitoa uamuzi Mwezi machi ulioamrisha makatibu hao kutopokea mishahara wala kutekeleza majukumu yoyote hadi pale kesi hiyo itakapo amuliwa