Rais William Ruto amewahakikishia wakenya kuwa serikali ya kitaifa itavipiga jeki vitengo vya afya kwa kufadhili ununuzi wa vifaa hitajika ili kuboresha huduma za afya

Katika mpango huo serikali kupitia bunge inapania  kuanzisha mradi wa Uboreshaji wa Vituo vya afya utakaolinda rasilmali zilizotengwa na kuboresha utaoji wa huduma.

“Tumekubaliana na serikali za kaunti ya kwamba tutakuwa na hazina maalum inayoitwa Facility Improvement Fund” alisema Rais William Ruto

Kiongozi wa taifa  alikuwa akizungumza katika ufunguzi rasmi wa hopsitali ya Rufaa ya Kerugoya huko Kirinyaga,

Rais aidha ameongeza  kuwa tayari serikali imetenga shilingi bilioni 15 ili kuwapiga jeki zaidi ya wahudumu 100,000 wa afya wa kujitolea watakaosaidia kufanikisha mpango huo.

“serikali ya Kenya itawaajiri wahudumu 100,000 wa kujitolea  ambapo  kila muuguzi atakua anasimamia familia mia moja” alisema Kiongozi wa Taifa

Kuhusu swala la bima ya afya NHIF rais amesema wakenya sasa  watapata afueni baada ya matozo ya bima hiyo kusawazishwa.

“Vile sasa tumeibadilisha mama mboga atalipa 2.7% na mimi nitalipa 2.7% ya mapato yangu”alisema Rais

Hata hivyo Rais ametetea hatma ya huduma za afya kutwaliwa na serikali za kaunti akisema huduma za afya zimezidi kuboreka zaidi na kuwapongeza wahudumu wa afya wanaojitolea ili kuhakiksha sekta ya afya inaimarika