Msajili wa mahakama Ann Amadi sasa anaweza kutumia akaunti zake zilizokuwa zimefungwa mwezi uliopita kufuatia kesi ya sakata ya dhahabu

Akitoa amri hiyo Jaji Alfred Mabeya amesema hakuna ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa Amadi alifaidi na shilingi milioni 100 alizodaiwa kulaghai kampuni ya Dubai, Bruton Gold Trading

“Hakuna chochote cha kuonyesha kwamba mshtakiwa wa kwanza (Bi Amadi) alihusika katika shughuli za kila siku za kampuni ya mawakili iliyohusika na madai ya ulaghai au ushahidi wa kuonyesha kwamba alinufaika na pesa hizo,” hakimu alisema.

Jaji Mabeya, hata hivyo, alikataa kusitisha kesi hiyo kama ilivyoombwa na Bi Amadi  na  mwanawe Brian Ochieng, ambaye alikiri kupokea mamilioni hayo kwa ununuzi wa dhahabu hiyo mnamo 2021.

Jaji alisema Bw Ochieng anafaa kubeba msalaba wake mwenyewe kwa sababu yeye ni mtu mzima.

Amadi, mwanawe Brian Ochieng na washukiwa wengine wawili kutoka kampuni ya uwakili ya Amadi Associates Advocates, wanadaiwa kulaghai kampuni ya Bruton Gold Trading kwa kukosa kuwasilisha dhahabu licha ya kupokea malipo