Rais William Ruto hii leo atakuwa anahudhuria mkutano wa 22 wa viongozi wa mataifa wanachama wa jumuiya ya soko la pamoja baina ya mataifa ya ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) utakaofanyika jijini Lusaka nchini Zambia. 

Mkutano huo unalenga  kukuza “Ushirikiano wa Kiuchumi wa soko la pamoja COMESA inayozingatia uwekezaji wa kijani, ongezeko la thamani na vilevile ukuzaji wa sekta ya utalii

Viongozi hao wa mataifa vilevile wanatazamiwa kujadili hali ya ushirikiano na utangamano baina ya wananchama wa  COMESA na  Pia maswala ya  usalama.

Ikumbukwe mnamo mwezi Mei tarehe 31 rais Ruto alihudhuria mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Bujumbura, Burundi ambapo hali ya usalama Mashariki mwa taifa la Demokrasia ya Congo ulijadiliwa