Kenya imejitolea kukaribisha viwanda zaidi vya kuunda magari ili kuongeza utengenezaji wa magari mapya nchini.
 Rais William Ruto alisema Sera ya Kitaifa ya Magari imetoa mazingira mwafaka kwa makampuni kuanzisha shughuli zao nchini Kenya.
 Alibainisha kuwa sera hiyo imedhibiti ukosefu wa utulivu katika sekta hiyo, hasa kuhusu sheria za kodi.
 “Mpango wetu ni kwa waundaji zaidi wa magari kuanzisha na kufanya kazi kwa uwezo kamili ili tuweze kuipatia Afrika magari kwa bei zenye kuhimili ushindani ulimwenguni,” alibainisha.
 Rais alisema hii itatoa nafasi nyingi zaidi za ajira, kukuza ujuzi na usafiri unaotegemeeka.
 Alisisitiza kuwa ni wakati umewadia kwa Kenya kuchukua nafasi yake halisi miongoni mwa wazalishaji wakuu wa magari barani Afrika.
Kiongozi wa Nchi aliyazungumza hayo siku ya Jumatano alipozindua mtambo wa kwanza kabisa wa kuweka rangi wa kielektroniki katika kiwanda cha Isuzu cha Afrika Mashariki.
 Inatarajiwa kwamba mtambo huo wa shilingi milioni 500 utaimarisha utengenezaji wa magari wa kampuni hiyo, kuboresha uzalishaji wa ndani na kuifanya iwe ya ushindani duniani kote.
 Viongozi waliohudhuria ni Mkurugenzi Mkuu wa Isuzu Afrika Mashariki Rita Kavashe, Katibu Mkuu wa Biashara Alfred K’Ombudo, Mwenyekiti wa Isuzu Afrika Mashariki Hiroshi Hisatomi, Naibu Mshauri Mkuu katika Ubalozi wa Japan Kitagawa Yasuhisha, miongoni mwa wengine.
 “Kwa uwekezaji kama huu wa kampuni ya Isuzu, tunaweza kurudisha Kenya kwenye ruwaza yake ya awali ya kuongoza ushindani wa utengenezaji magari barani Afrika.”
 Rais aliwataka wawekezaji kuendeleza uwekezaji wao nchini Kenya kwa kuingia katika kitengo cha Daraja la Kwanza la utengenezaji.
 Alisema Kenya inanuia kutumia kikamilifu fursa kubwa itokanayo na sekta ya magari ambayo haijatumika.
 Bw Yasuhisha alibainisha kuwa uwekezaji wa Isuzu utachochea uhamisho wa teknolojia, ujuzi na utaalamu.
 “Pia inakuza utengenezaji wa mazingira safi wakati ulimwengu unakabiliwa na mabadiliko ya tabianchi.”
 Kwa miaka minne sasa, Isuzu East Africa imewekeza shilingi bilioni 1.3 katika upanuzi na uboreshaji, hivyo imetoa ishara wazi ya imani yake kwa Kenya kama kivutio cha uwekezaji.Kenya imejitolea kukaribisha viwanda zaidi vya kuunda magari ili kuongeza utengenezaji wa magari mapya nchini.

Rais William Ruto alisema Sera ya Kitaifa ya Magari imetoa mazingira mwafaka kwa makampuni kuanzisha shughuli zao nchini Kenya.

Alibainisha kuwa sera hiyo imedhibiti ukosefu wa utulivu katika sekta hiyo, hasa kuhusu sheria za kodi.

“Mpango wetu ni kwa waundaji zaidi wa magari kuanzisha na kufanya kazi kwa uwezo kamili ili tuweze kuipatia Afrika magari kwa bei zenye kuhimili ushindani ulimwenguni,” alibainisha.

Rais alisema hii itatoa nafasi nyingi zaidi za ajira, kukuza ujuzi na usafiri unaotegemeeka.

Alisisitiza kuwa ni wakati umewadia kwa Kenya kuchukua nafasi yake halisi miongoni mwa wazalishaji wakuu wa magari barani Afrika.

Kiongozi wa Nchi aliyazungumza hayo siku ya Jumatano alipozindua mtambo wa kwanza kabisa wa kuweka rangi wa kielektroniki katika kiwanda cha Isuzu cha Afrika Mashariki.

Inatarajiwa kwamba mtambo huo wa shilingi milioni 500 utaimarisha utengenezaji wa magari wa kampuni hiyo, kuboresha uzalishaji wa ndani na kuifanya iwe ya ushindani duniani kote.

Viongozi waliohudhuria ni Mkurugenzi Mkuu wa Isuzu Afrika Mashariki Rita Kavashe, Katibu Mkuu wa Biashara Alfred K’Ombudo, Mwenyekiti wa Isuzu Afrika Mashariki Hiroshi Hisatomi, Naibu Mshauri Mkuu katika Ubalozi wa Japan Kitagawa Yasuhisha, miongoni mwa wengine.

“Kwa uwekezaji kama huu wa kampuni ya Isuzu, tunaweza kurudisha Kenya kwenye ruwaza yake ya awali ya kuongoza ushindani wa utengenezaji magari barani Afrika.”

Rais aliwataka wawekezaji kuendeleza uwekezaji wao nchini Kenya kwa kuingia katika kitengo cha Daraja la Kwanza la utengenezaji.

Alisema Kenya inanuia kutumia kikamilifu fursa kubwa itokanayo na sekta ya magari ambayo haijatumika.

Bw Yasuhisha alibainisha kuwa uwekezaji wa Isuzu utachochea uhamisho wa teknolojia, ujuzi na utaalamu.

“Pia inakuza utengenezaji wa mazingira safi wakati ulimwengu unakabiliwa na mabadiliko ya tabianchi.”

Kwa miaka minne sasa, Isuzu East Africa imewekeza shilingi bilioni 1.3 katika upanuzi na uboreshaji, hivyo imetoa ishara wazi ya imani yake kwa Kenya kama kivutio cha uwekezaji.