Maafisa wa polisi wamelazimika kutumia vitoza machozi ili kuwatawanya mamia ya wanaharakati walioandamana katikati mwa jiji la Nairobi ili kupinga mswada wa  fedha wa 2023/2024

Wanaharakati hao kutoka mashirika ya kutetea haki za binadamu walianza matembezi katika bustani la Jevanjee wakielekea katika majengo ya bunge wakiwa wamebeba mabango ya kupinga mswada huo

Imeripotiwa kuwa baadhi ya waandamanaji wametiwa mbaroni baada ya kukabiliwa na maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria

Katika mswada huo unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni ili kujadiliwa wakenya wengi wameendelea kulalamikia ikiwemo pendekezo la makato ya asilimia tatu ya mishahara ya wafanyikazi walioajiriwa ili kugharamia mradi wa serikali wa nyumba za bei nafuu