Baadhi ya wandani wa Kinara wa Azimio One Kenya Raila Odinga sasa wametangaza kutambua uhalali wa ushindi wa Rais William Ruto kinyume na rai za Odinga kwa wakenya Kupinga utawala wa Ruto. 

Odinga katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa katika uwanja wa Kamkunji alishikilia kua aliibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu ulioandaliwa Agosti tisa akinukuu mfichuzi anayedai kua mfanyikazi wa IEBC aliyedai kua Odinga alimbwaga Rais Ruto kwa kuzoa asilimia 57.53 ya kura zilizopigwa ikilinganishwa na 41.66 alizopata Ruto

Hata hivyo aliyekua mbunge wa Mukurwe-ini Kabando wa Kabando ameshikilia kua licha ya kua mwanachama wa muungano wa Upinzani anatambua uhalali wa ushindi wa Rais Ruto.

Kabando aliyewania kiti cha Useneti wa Kaunti ya Nyeri kwa Tikiti ya Chama cha NARC Kenya ametilia shaka iwapo Rais mstaafu Uhuru Kenyatta na viongozi wa vyama tanzu vya muungano wa Azimio One Kenya walishauriwa kabla ya Odinga kuafikia uamuzi wa kutotambua ushindi wa Rais Ruto.

Aliyekua Ajenti Mkuu wa Odinga katika Uchaguzi Mkuu uliopita Saitabao Kanchorry kwa upande wake ametaka Kinara huyo wa Upinzani kutoa mwelekeo kuhusu hatua Azimio itachukua la sivyo afiate mdomo.

Kanchorry anahoji kua Wakenya wamechoka na michezo ya kisiasa anayofanya Odinga.

Odinga, katika Mkutano ulioandaliwa katika uwanja wa Kamkunji siku ya jana miongoni mwa mambo mengine   alitaka Wakenya kususia kulipa kodi akidai kua Serikali ya Kenya Kwanza sio halalai.