Rais william Ruto pamoja na Rais Cyril Ramaphosa katika ikulu ya Rais

Alipowasili katika ikulu ya Rais jijini Nairobi , Rais Ramaphosa alipokelewa na mwenyeji wake Rais William Ruto na kupigiwa mizinga ishirini na moja na maafisa wa jeshi la KDF kama ishara ya heshima kwa kiongozi huyo.

Marais hao na wajumbe wao kwa sasa wanafanya mazungumzo kabla ya kuhutubia kikao cha pamoja na wanahabari.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa  kuimarisha uhusiano kati ya taifa la Kenya na Afrika Kusini na pia njia za kurahisisha upatikanaji wa vyeti kwa wakenya wanaotaka kuzuru Afrika Kusini.

Rais Ramaphosa anatarajiwa pia kuhudhuria  mkutano wa kibiashara na uwekezaji baina ya Kenya na Afrika Kusini katika Jumba la kimataifa la mikutano, KICC.

Rais Ramaphosa aliwasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta Jumanne usiku na kupokelewa na waziri wa mambo ya nje Alfred Mutua na mwenzake wa uchimbaji wa madini Salim Mvurya.