Chama cha UDA chake   Rais William Ruto kimejitenga na pendekezo la kubadilisha kipengee cha sheria kinachomzuia Rais kuwa madarakani kwa zaidi ya mihula miwili ya miaka tano.

Mwenyekiti wa UDA Johnson Muthama amesema pendekezo hilo lake mbunge wa Fafi Salah Yakub ni msimamo wake kibinafsi wala sio   msimamo wa chama akisema chama hicho kinapendelea mpangilio uliopo sasa  ambapo Rais anaongoza kwa kipindi kisichozidi  mihula miwili ya miaka tano.

Baadhi wa ndani wa Rais William Ruto akiwemo Mwanablogu Denis Itumbi, Miguna Miguna na Senta Khalwale wamekashifu pendkezo hilo wakisema Kiongozi wa Taifa haiungi mkono.

Kupitia akaunti yake ya Twita Wakili Miguna amesema iwapo Rais William ruto ataunga mkono mpango huo; atakosa ungwaji mkono wa wakenya wengi na huenda akashindwa kutwa urais kwa mara ya Pili.

” Mpango huo ni utani usiofaa hata kidogo. Wakenya hawawezi kupitisha pendekezo hilo   katika kura ya maoni. Pandekezo hilo litamfanya Ruto kua rais wa kwanza kuhudumu muhula mmoja,” alisema Miguna.

Mbunge huyo anasema tayari mapendekeo yake yamepokelewa vema na wabunge wa UDA na atawasilisha mswada huo wa marakebisho bungeni hivi karibuni.