Viongozi wa Muungano wa Marubani wa KQ wakihutubia wanahabri

Mahakama imeagiza marubani wa kampuni ya ndege ya Kenya Airways (KQ) kurejea kazini kufikia saa kumi na mbili  asubuhi siku ya Kesho. 

Jaji wa mahakama ya Leba Anne Mwaure aidha ametaka Usimamizi wa Kampuni ya KQ kutochukua hatua zozote za kinidhamu dhidi ya marubani hao waliogoma.

Uamuzi huo uliafikia baada ya Jaji Mwaure kuagiza pande zote kujadiliana na kupata mwafaka kuhusu mgomo huo.

Mahakama hii inaagiza muungano wa marubani KALPA kuhakiksiha kua wanachama wake wanarejea kazini kabla ya saa kumi na mbili asubuhi tarehe 9 Novemba mwaka huu. Mwajiri wao anaagizwa kutowachukulia hatua marubani waliogoma.” Ameagiza Mwaure.

KQ imetakiwa kuwasilisha majibu yake kabla ya 15 Novemba kesi hio ikitarajiwa kuskizwa 21 novemba mwaka huu.

Shirika la waajiri FKE  mapema hii leo kilitaka usimamizi wa Kampuni ya Ndege KQ sawia na muungano wa marubani KALPA kutatua tofauti kati yao ili kusitishwa kwa mgomo unaoendelea.

Mgomo huo ambao umelemeza shughuli za usafiri humu nchini umeingia siku ya nne KQ kikidai kinakadiria hasara ya zaidi ya shilingi milioni mia tatu kila siku marubani nao   wakiapa kutorejea  angani mpaka matakwa  yao yatimizwe