Rais Uhuru Kenyatta amemtuma waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i kupeleka ujumbe maalum kwa rais mpya wa Zambia Hakainde Hichilema.

Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna kupitia ujumbe wa Twitter ameeleza kuwa mataifa haya mawili yanafurahia uhusiano wa karibu na hivyo umuhimu wa ujumbe maalum kufikishwa.

Ujumbe huo ni pamoja na kuwa na ushirikiano mpya na kuomba Zambia kuunga mkono Kenya kwenye azma yake ya kuwa katibu mkuu kwenye Jumuiya ya Madola (Common Wealth).

Juma lililopita, rais Kenyatta aliandamana na kinara wa upinzani Raila Odinga kuhudhuria hafla ya uapisho wa Hakainde.