Tume ya usawa wa jinsia nchini (NGEC) imeadhimisha miaka kumi tangu kubuniwa kwake kushinikiza kuwepo kwa usawa katika nafasi za uongozi.

Akihojiwa na kituo na www.bibliahusema.org, kamishna wa tume hiyo Priscilla Nyokabi anasema wanajivunia hatua walizopiga tangu kubuniwa kwao ikizingatiwa kwamba idadi ya wanawake na walemavu walio katika nafasi za uongozi imeongezeka.

Hata hivyo tume hiyo inahoji kwamba juhudi zaidi zinapaswa kuwekwa katika uchaguzi mkuu ujao ili kuhakikisha kwamba sheria ya usawa ambayo bado haijatekelezwa inaafikiwa kikamilifu.