Viongozi wa kidini wanamtaka rais Uhuru Kenyatta kupatana na naibu wake William Ruto kwa manufaa ya amani ya taifa hili.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa muungano wa makanisa ya kipentekote nchini Stanley Michuki, viongozi hao wanahoji kwamba tofauti baina ya rais na mdogo wake zinafaa kusuluhusihwa haraka upesi kwani Wakenya wanaumia.

Wamesema wataongoza juhudi za kuwapatanisha wawili hao licha ya juhudi za hapo awali kuonekana kukosa kuzaa matunda.

Mwenzake askofu Tee Nalo ambaye ni mkurugenzi wa makanisa ya kipentekote anasema sawa na rais alivyopatana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, ndivyo wanapaswa kupatana na naibu wake ili kuwe na amani nchini.

Kauli hizi zinawadia siku chache baada ya rais kumtaka naibu wake kujiuzulu ujumbe ambao Ruto aliupuuza na ikafuatia hatua ya serikali kumpkonya naibu rais walinzi wa GSU katika makaazi yake.