Kamati ya BBI imesema itaunga mkono rufaa ya mwanasheria mkuu Paul Kihara katika mahakama ya upeo kuhusu mchakato wa kurekebisha katiba kupitia BBI.

Wenyekiti wenza wa kamati hiyo Dennis Waweru na Junet Mohamed ambao wameapa kufuatilia BBI hadi mwisho wanasema majaji wa mahakama ya juu zaidi nchini ndio wana usemi wa mwisho kuhusu maswala yenye umuhimu yaliyaomuriwa na mahakama ya rufaa.

Kamati hiyo inahoji kwamba taifa litajipata kwenye njia panda kikatiba iwapo baadhi ya mapendekezo kwenye mswada huo ikiwemo kuafikiwa kwa usawa wa jinsia hayatatekelezwa.

Tayari mwanasheria mkuu Paul Kihara amesema ataelekea katika mahakama ya upeo kupinga uamuzi huo uliosimamisha marekebisho ya katiba kupitia BBI.