Waziri wa Usalama wa ndani Fred Matiang’i ametoa wito kwa vijana kukataa kutumiwa na wanasiasa kuzua vurugu haswa msimu wa kampeni za uchaguzi unapokaribia.

Akizungumza huko Limuru wakati wa kongamano ambalo limeandaliwa na baraza la makanisa nchini NCCK, Matiang’i anasema iwapo vijana watakataa kutumiwa vibaya na wanasiasa, taifa litakuwa na uchaguzi huru na wa amani.

Akionekana kurejelea mfumo wa uchumi anaotumiwa naibu Rais William Ruto kujipigia debe, Matiang’i amesema taifa linahitaji uongozi ambao utatoa suluhu kwa changamoto zinazolikumba taifa.