Benki ya Equity imekana madai yaliyotolewa na naibu rais William Ruto kwamba ilimpatia mkopo wa shilingi billion kumi na tano raia wa Uturiki Harun Aydin aliyefurushwa nchini.
Akifika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu fedha inayoongozwa na mbunge wa Homabay Gladys Wanga, mkurugenzi mkuu wa Equity Gerald Warui amesema benki hiyo haina uhusiano wowote wa kibiashara na Aydin.
Warui amekana madai ya Ruto Ruto kuwa aliwapigia simu na kutaka wamsaidie Aydin kupata pesa hizo ili kumsaidia kufanya biashara nchini Uganda.
Ruto alidai kwamba alipigia Eqity Bank simu ili wampatie Aydin mkopo ili awekeze katika taifa jirani la Uganda.
Aydin alifaa kuandamana na Ruto kueleka nchini Uganda mwezi uliopita, safari ambayo iligonga mwamba.