Watumishi wa umma nchini Kenya wana hadi hii leo Jumatatu Agosti 23 kupata chanjo dhidi ya corona la sivyo wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Makataa yaliyotolewa na mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinyua yanaisha leo Agosti 23.

Wafanyikazi wa serikali wanakabiliwa na tishio la kunyimwa mishahara na marupurupu iwapo watakosa chanjo hiyo kwa mujibu wa naibu katibu mkuu wa utumishi wa umma Mary Kimonye.

Serikali kupitia kwa msemaji wake kanali mstaafu Cyrus Oguna imetetea hatua hiyo ikisema baadhi ya watumishi wa umma walikuwa wanatumia chanjo kama kijisababu kuheba kazi.