Baraza la Magavana limesema litashirikiana na bunge kushinikiza marekebisho ya katiba ili mgao wa serikali za kaunti kuongezwa.
Hii ni baada ya kuanguka kwa marekebisho ya katiba kupitia mchakato wa BBI kusimamishwa na bunge.
Kamati ya baraza hilo la magavana kuhusu maswala ya kisheria inasema baadhi ya marekebisho hayo ya katiba yanaweza yakarekebishwa kupitia bunge na wala sio kura ya maamuzi.
Hayo yakijri
Waziri wa Mawasiliano (ICT) Joe Mucheru ameikosoa mahakama ya rufaa kwa kusitisha mchakato wa BBI.
Akizungumza kwenye kongamano la vijana la muungano wa makanisa inchini (NCCK), Mucheru amesema marekebisho hayo yalikuwa na malengo ya kuwafaidi vijana.
Akionekana kumlenga naibu rais William Ruto, Mucheru amesema wanaosherehekea uamuzi huo wa mahakama ya rufaa walikosa kuona manufaa ya BBI kwa taifa.