Naibu rais William Ruto sasa anasema chama cha United Democratic Alliance (UDA) kimeleta mwamko mpya wa kisiasa nchini pasipo ukabila.

Akizungumza alipokutana na wawaniaji mbalimbali kutoka Nairobi katika afisi zake zilizoko Karen Jumatano, Ruto amesema chama hicho kitatatua changamoto zinazowakumba Wakenya ikiwemo uchumi.

Ruto vile vile ameendelea kushambulia handisheki baina ya rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga kwa kusababisha matatizo yanayolikumba taifa wakati huu.