Maseneta wamemuomboleza mwenzao wa kuteuliwa Victor Prengei aliyefariki baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani Nakuru Jumatatu usiku.

Wakimuomboleza marehemu baada kuutizama mwili wake katika hifadhi ya Lee Jumatano, maseneta wakiongozwa na spika Ken Lusaka wamemtaja Prengei kama mchapa kazi aliyefanya kazi kwa kujitolea.

Seneta Prengei, 36, alikuwa seneta wa kwanza kutoka jamii ndogo ya Ogiek na aliwawakilisha vijana bungeni.