Polisi huko Kitengela kaunti ya Kajiado wanachunguza kisa ambapo mama mmoja alimuaa mwanawe mwenye umri wa miaka miwili kabla ya kujinyonga ndani ya nyumba yao.
Baada ya kumuua mwanawe, Jane Wairimu Macharia aliingia bafuni na kujinyonga na kuacha barua yenye madai ya kumlaumu mumewe kwa kutokuwa mwaminifu.
Mama huyo anasemekana kumtuma mfanyikazi wao wa nyumbani kabla ya kujifungia chumbani mwao na kutekeleza mauaji hayo na kisha kumuweka mwanawe kitandani.
Akidhibitisha tukio hilo, kamanda wa Polisi kaunti ndogo ya Isinya Charles Chepkonga amesema mumewe marehemu alikuwa kazini wakati mkewe alimuua mwanawe na kisha kujitoa uhai.