Idadi ya wagonjwa wa corona wanaohitaji hewa ya oxijeni katika hospitali mbalimbali inazidi kuongezeka huku taifa likiandikisha maambukizi zaidi ya ugonjwa huo.

Wizara ya afya inasema wagonjwa 1,970 wamelazwa hospitalini huku 147 wakiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Kutokana na haja hii, serikali za kaunti zimetakiwa kujitahidi kupata hewa hiyo ili kuokoa maisha ya wanaohitaji.

Katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita, maambukizi mapya 1,488 yamedhibitishwa nchini baada ya kupima sampuli 9,773 huku kiwango cha maambukizi kikiwa asilimia 15.2%.

Watu wengine 1,814 wamepona huku 4 zaidi wakifariki na kufikisha idadi ya maafa kuwa 4,354.