Mshukiwa mkuu wa mauaji ya watu wanne mtaani Kitengela wiki iliyopita atazuiliwa kwa muda wa siku kumi zaidi.

Hii ni baada ya mahakama kuiridhia ombi la polisi kumzuilia Benson Melonyie ole Mungai, 40 ili kukamilisha uchunguzi.

Upande wa mashtaka unasema una ushahidi wa kutosha kudhibitisha kuwa mshukiwa alihusika katika mauaji ya wanne hao ambao walisingizwa kuwa wezi wa mifugo.

Melonyie alikamatwa jana jioni kutoka mafichoni mjini Kitengela ambapo inaaminika amekuwa akijficha tangu kudaiwa kuongoza mauaji ya wanne hao Fred Mureithi, Victor Mwangi, Mike George, na Nicholas Musa.

Mshukiwa anatazamiwa kufikishwa mahakamani hii leo ambapo polisi wataomba muda zaidi kumzuilia huku uchunguzi zaidi ukifanyika.