Waanzilishi wa vuguvugu la kisiasa la kuunganisha eneo la Mt. Kenya kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022 wameelezea matuamini yao kwamba watafaulu kwenye azimio lao.

Watatu hao mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria, aliyekuwa waziri Mwangi Kiunjuri na kiongozi wa chama cha NARC K Martha Karua wanasisitiza kwamba eneo hilo ni sharti lizungumze kwa sauti moja kabla uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.