Hali ya huzuni na majonzi imetanda katika eneo la Kianjokoma kaunti ya Embu wakati wa mazishi ya ndugu wawili waliofariki mikononi mwa Polisi baada ya kushikwa kwa kudaiwa kupatikana nje wakati wa kafyuu.

Safari ya wawili hao Benson Njiru,22 na Emmanuel Mutura,19 imeishia katika kaburi la pamoja Kithangari huku viongozi mbalimbali wakiongozwa na spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi wakitaka haki kutendeka.

Miili ya wawili hao ilipatikana katika hifadhi ya hospitali ya Embu Level 5 siku tatu baada ya kukamatwa.

Upasuaji ulionesha kwamba wawili hao walikuwa na majeraha vichwani na kwenye mabega.