Magari ya uchukuzi wa umma yamerejelea kubeba abiria kama ilivyokuwa kabla ya janga la covid-19.
Wahudumu wa matatu wanatakiwa kuhakikisha kuwa abiria wanavalia barakoa na pia kuweka vieuzi vya kutakasa mikono
Hatua hii ina maana kuwa starehe za abiria kukaa umbali wa angalau mita moja kutoka kwa wenzao, kuzuia uwezekano wa kuambukizana virusi vya corona, imefikia kikomo.
Hata hivyo abiria waliotarajia kupunguzwa kwa nauli huenda wasipate afueni hiyo baada ya wahudumu wa matatu kusema hawatapunguza nauli kutokana na bei za juu za mafuta.
Wizara ya uchukuzi imeonya matatu zitakazopatikana zikikaidi maagizo hayo zitapigwa marufku kuhduumu.