Uganda sasa inasema haikujulishwa kuhusu ziara ya naibu rais William Ruto iliyotibuliwa na serikali Jumatatu.

Waziri wa mambo nje wa Uganda Okello Oryem anasema hawangeweza kupanga itifaki ya Ruto kwa sababu hawakuwa na ufahamu kuhusu ziara yake.

Kampala vile vile imekana kuingilia kwa vyovyote maswala ya ndani ya Nairobi na kusema wanaheshimu maamuzi yanayofanywa na taifa hili.

Oryem amewataka wanaowauliza maswali kuhusu safari ya Ruto ambayo iliishia kwenye uwanja wa ndege kutafuta majibu ya maswali yao kwa wizara ya masuala ya kigeni ya Kenya.