Mkenya Nicholas Kimeli amefuzu kwenye fainali za mita 5,000 kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea mjini Tokyo, Japan.

Kimeli anatazamiwa kupambana na Mohammed Ahmed wa Canada na Oscar Chelimo wa Uganda kwenye fainali Ijumaa hii.

Matarajio ya Wakenya wengi ni kwamba Kimeli ataishindia Kenya medali zaidi kwenye fainali hizo kama walivyofanya Hellen Obiri na Benjamin Kigen.  

Kigen alishinda medali ya SHABA baada ya kumaliza wa tatu kwenye mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji.

Hellen Obiri aliishindia Kenya nishani ya pili baada ya kumaliza wa pili na kushinda FEDHA kwenye mbio za mita 5,000 kwa wanawake.