Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amesifia uamuzi wa chama cha ODM kujinasua kutoka kwa uliokuwa muungano wa upinzani nchini NASA.

Kuria kupitia kwa ukurasa wake wa Facebook amesema kujiondoa kwa NASA ndio uamuzi muhimu ambao Raila Odinga amewahi kufanya.

Mwendani huyo wa naibu rais William Ruto amesema washirika wengine kwenye muungano huo Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Moses Wetangula kwa muda mrefu wamekuwa wakimpanda Raila kwa mgongo.

Haya yanajiri siku moja baada ya baraza kuu la chama ODM kuidhinisha uamuzi wa kujiondoa rasmi kwa NASA kutokana kile limetaja kama ukosefu wa uaminifu.