Chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga kimetangaza mipango ya kujiondoa rasmi kwenye uliokuwa muungano wa upinzani nchini NASA.
Katibu mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna ametangaza hili baada ya mkutano wa baraza kuu NEC ulioidhinisha uamuzi wa kujiondoa kwa muungano huo.
Sifuna amesema wameamua kuachana na NASA kwa sababu ya ukosefu wa uaminifu miongoni mwa washirika wake.
Haya yanajiri siku chache baada ya chama cha Wiper kinachoongozwa na Kalonzo Musyoka kutangaza kujitoa kwa NASA baada ya baraza kuu la chama hicho kuidhinisha uamuzi huo.