Mkewe rais Margaret Kenyatta ameelezea umuhimu wa kuwepo kwa haja ya kuwekwa juhudi za pamoja kukabiliana na changamoto ya matatizo ya kiakili.

Bi. Kenyatta amesema sawa na matatizo mengine ya kiafya yanavyopewa kipau mbele, afya ya akili inafaa kumulikwa hata na zaidi kwa sababu ina tiba.

Mkewe rais amesema licha ya kuwa na tiba, wengi ya wanaougua magonjwa ya kiakili wameachwa kuhangaika na hivyo kuishia kuharibu maisha yao kwa kugeukia dawa za kulevya.

Ameongeza kuwa hali imekuwa mbaya kufuatia janga la corona na hivyo kuongeza idadi ya waliopatwa na matatizo yta kiakili.