Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua ameachiliwa kwa dhamana ya Sh12M pesa taslimu au mdhamini wa Sh25M baada ya kukanusha mashtaka ya ufisadi dhidi yake.

Gachagua amefikishwa mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Lawrence Mugambi ambapo amekanusha kupanga njama na washukiwa wengine kuibia serikali ya kaunti ya Nyeri Sh27M kati ya mwaka 2013-2020.

Mahakama imeamuagiza Cachagua kuwasilisha pasipoti yake mahakamani huku washukiwa wenzake tisa wakitafutwa.

Mbunge huyo amekabiliwa na mashtaka sita ikiwemo wizi wa mali ya umma, utumizi mbaya wa afisi na ulanguzi wa pesa.

Mbunge huyo ambaye amewasilishwa mahakamani na mawakili kumi ameomba mahakama kumuachiliwa kwa dhamana.