Kumetokea maandamano kwenye barabara kuu ya Nyeri-Nairobi kupinga kukamatwa kwa mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua.
Iliwalazimu Polisi wa kupambana na ghasia kutumwa ili kuzima maandamano hayo yaliyotatiza usafiri kwenye barabara hiyo.
Gachagua alishikwa mapema Ijumaa nyumbani kwake Nyeri na kupelekwa katika makao makuu ya idara ya uplelezi (DCI) kuhojiwa kwa madai ya ufisadi.
Wapelelezi wa DCI wanachunguza sakata ya Sh12b zinazohusishwa na akaunti za mbunge huyo.
Mbunge huyo amekaribisha hatua ya kukamatwa kwake akisema inampa nafasi ya kusafisha jina lake mahakamani kuhusiana na tuhuma zinazomkabili.
Hata hivyo mbunge huyo anaendelea kusema kukamatwa kwake kumechochewa na mchango wake katika uchaguzi mdogo wa eneobunge la Kiambaa.