Jaji Mkuu Martha Koome sasa anasema hajui chochote kuhusu kukamatwa kwa majaji wawili Aggrey Muchelule na Said Juma Chitembwe kwa tuhuma za ufisadi.

Katika taarifa, Koome amesema hakuna malalamishi yoyote kuwahusu majaji hao ambayo yamewasilishwa kwake kama kiongozi wa idara ya mahakama na mwenyekiti wa tume ya huduma za mahakama (JSC).

Koome hata hivyo amewarai maafisa wa mahakama kuendelea na majukumu yao bila woga huku akiapa kuendelea kulinda uhuru wa idara ya mahakama.

Idara ya upelelezi (DCI) inasema wawili hao wamehojiwa na kuandikisha taarifa kwa tuhuma za ufisadi na kwamba uchunguzi unaendelea.

Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Hajji amekanusha ripoti kuwa aliagiza kukamatwa kwa Muchelule na Chitembwe.

Wakati uo huo